Wilaya ya Mjini ikiendelea na Mikakati yake ya kuhakikisha inaboresha mazingira ya wajasiriamali kwa maeneo tofauti ili kukuza uchumi, kuongeza kodi kwa kuvutia mazingira ya kupata vyanzio vipya vya kodi, kuongeza harakati za kijamii na ubunifu kwa wafanyabishara ili kukuza biashara zao.
Wilaya ya Mjini imeweka historia mpya ya kuondosha wafanyabiashara wa Darajani kwa muda bila kutumia nguvu ya aina yoyote ili kupisha ukarabati wa Soko kuu la Darajani. Soko hilo litafanyiwa ukarabati mkubwa ambao haukuwahi kufanyika kabla. Ukarabati huo utafanya na kampuni ya Simba Developers na utachukua muda wa miezi 2 tu.
Haya yote ni miongoni ya Ahadi za Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi la kuhakikisha wajasiriamali kuboreshewa maeneo yao ya biashara.