Tumefarijika kwa kutembelea na kuzinduliwa Kampeni ya Nitunze katika Bustani ya Botanic ilioko Migombani na Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Mama Mariam Mwinyi.
Kampeni hio ni miongoni mwa Utekelezaji wa Maagizo ya Mhe. Rais ya Kuendelea kuibua miradi, vyanzo vipya vya Mapato na pia Vivutio vipya vya Utalii.
Miongoni mwa mambo alioyaongea Mama na kuyaagiza kwa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale ni kuisimamia bustani ile na inawezekana ikawa bustani ya kuvutia kama ilioko Singapore.