Katibu Tawala Wilaya ya MjiniĀ Dkt Said Haji Mrisho alifanya kikao na Uongozi wa Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amani. Kikao ambacho kilikusudia kuangalia fursa mbali mbali ambazo Wilaya inaweza kufaidika pindi iki shajihisha Wananchi kuchangia katika mifuko ya Zakka, Sadaka, na Misaada ya kheir ikiwemo elimu, afya n.k
Miongoni mwa Maazimio ni kufanya Kikao na na Jumuiya ya wafanyabisha wa Darajani tarehe 17/11/2022 ambacho Wilaya imeahidi kuwaita. Vile vile kuendelea na kushajihisha watu wengine ndani ya Wilaya ikiaanza na Wafanyakazi wetu wa ndani pamoja na Waheshimiwa Masheha.