Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi leo alifanya ziara katika Hospitali ya Mkoa wa Mjini katika eneo la Lumumba.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya alimpokea Mheshimiwa Rais kwa Niaba ya Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa na kupewa maelezo ya Kitaalamu na Mhandisi chini ya Kampuni Estim Enterprise na Waziri wa Afya pamoja na Naibu wa Waziri wa Afya.
Mheshimiwa Rais alipongeza sana hatua ya ujenzi na Kuendelea kutupatia Maagizo na Maelekezo Ili kuikamilisha Hospitali ya Mkoa na hadhi yake.